1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Askari kwenda Somalia

15 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cc7B

MOGADISHU.Burundi itatuma kikosi cha kwanza nchini Somalia mwezi huu kuungana na kile cha Uganda chini mwavuli wa Umoja wa Afrika kusaidia kulinda amani nchini humo.

Kikosi hicho kiutaungana na askari 1,600 wa Uganda waliyoko katika mji mkuu Mogadishu toka mwezi March mwaka huu.

Burundi iliahidi kupeleka askari 1,700 katika jeshi hilo la kulinda amani la Umoja wa Afrika, toka mwezi Julai lakini kutokana na uhaba wa vifaa pamoja na fedha imeshindwa kufanya hivyo.

Mjumbe maalum wa Umoja wa Afrika nchini Somalia, Nicolas Bwakira amesema kuwa mbali ya Burundi pia wanategemea askari kutoka Nigeria kuwasili nchini Somalia mnamo miezi miwili au mitatu ijayo.

Hali nchini Somalia hususani mjini Mogadishu imekuwa mbaya katika siku za hivi karibuni ambapo watu 18 walikufa kutokana na mashambulizi ya maroketi mjini humo juzi na jana.

Wapiganaji wa muungano wa mahakama za kiislam ambao walifurushwa na majeshi ya Ethiopea yanayoisaidia serikali ya mpito wamekuwa wakifanya mashambulizi mara kwa mara.