1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Asilimia 80 ya Wajapan wapinga Michezo ya Olimpiki

17 Mei 2021

Zaidi ya asilimia 80 ya Wajapan wanapinga kuandaliwa mwaka huu kwa michezo iliyoahirishwa ya Olimpiki, hatua inayoashiria upinzani wa umma kwa michezo hiyo

https://p.dw.com/p/3tV4P
Japan Tokio | Protest gegen Olympische Spiele
Picha: Kyodo/REUTERS

Japan imerefusha hali ya dharura ya janga la corona wakati nchi hiyo ikipambana na wimbi la nne. Uchunguzi wa maoni wa gazeti la Asahi Shimbun ulikuta kuwa asilimia 43 ya waliohojiwa wanataka michezo hiyo ifutwe, huku asilimia 40 wakitaka iahirishwe kwa mara nyingine. Takwimu hizi ni juu kutoka asilimia 35 waliounga mkono kufutwa katika utafiti wa mwezi uliopita, na asilimia 34 waliotaka iahirishwe tena.

Na wakati viongozi wa olimpiki wakijikuna kichwa, Rais wa chama cha riadha ulimwenguni Sebastian Coe amesema Ijumaa kuwa ana matumaini michezo hiyo itaendelea mwaka huu kama ilivyopangwa.

Amesema chanjo za covid-19 zinawapa wanamichezo fursa nzuri ya kuingia mazoezini na kushiriki mashindano ya kabla ya Olimpiki "Ninaamini kabisa tunaweza kuandaa tamasha hilo kwa njia salama. Hakuna suluhisho bora zaidi na kutakuwa na changamoto kubwa sana, lakini, maoni yangu halisi baada ya kuzuru Tokyo na mjini Sapporo ni kwamba itifaki hizi ni muhimu sana."

AFP/Reuters/DPA/AP