1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUganda

Asilimia 70 ya wafanyakazi wameajiriwa bila kandarasi Uganda

1 Mei 2023

Asilimia kubwa ya wafanyakazi hawana mikataba na waajiri wao, hali inayowapa waajiri uhuru wa kuwafuta kazi wafanyakazi wakati wowote na pia kutokuwajibika.

https://p.dw.com/p/4QkRN
Uganda führt drakonisches Anti-Schwulengesetz ein
Picha: Abubaker Lubowa/REUTERS

Kwa kuwa watu aslimia 70 ya wafanyakazi nchini Uganda hawana mikataba na waajiri wao, wananyimwa haki zao msingi kunufaika na jasho lao na maslahi yao hayazingatiwi ipasavyo na waajiri.

Kulingana na ripoti rasmi ya serikali, hii ni kinyume na sheria za nchi kwani makampuni hupendelea kufanya hivyo ili kukwepa kulia kodi za mapato za wafanyakazi na kugharimia maslahi ya wafanyakazi wao.

Hali hii inakinzana kabisa na kauli mbiu ya mwaka huu kwamba kukuza utamauduni maadili chanya ndicho chanzo cha kuzidisha uwekezaji, fursa za ajira na mapato kwa familia. 

Ijapokuwa kuna sheria inayomtaka mwajiri kuwa na mkataba na wafanyakazi ana kuwasilisha michango yao kwa shirika la mafao la NSSF, ni asli mia 30 tu ya waajiri hufanya hivyo. Lakini kwa nini watu wakubali kuajiriwa bila kuwa na mkataba na waajiri wao?

Kwa mtazamo wake, Dkt Akech serikali na hata waajiri wenyewe wanapata hasara kutokana na kutowapa wafanyakazi wao mkataba kwani wengi wao hukosa moyo  wa kuwa waaminifu na kujitolea ipasavyo kwa kazi zao kwa sababu wanajua kwamba wakati wowote wanaweza kufutwa kazi, yaani hawathaminiwi na waajiri.

Kiwango cha chini cha mshahara

Kwa upande wa mishahara, asilimia 60  ya wafanyakazi Uganda hupata shilingi laki mbili sawa na dola 60 hivi za kimarekani baada ya makato mmbalimbali ikiwemo kodi. Hizi pesa kwa wengi haziwezi kukidhi mahitaji yao msingi wala ya familia zao.

Ndiyo maana wadau wanaelezea kuwa ndicho chanzo cha wafanyakazi hao kushiriki katika ulaji rushwa na wengine kuhusika katika wizi wa mali za waajiri wao au kufanya kazi na biashara zingine ambazo huathiri utendaji kazi wao.

Takwimu pia zinaonyeha kuwa mwaajiri mmoja Uganda hutegemewa na watu watano kwani kati ya idadi ya watu milioni 45 hivi ni milioni tisa tu walio na njia hakika za kipato.