1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ASEAN wakutana kujadili usalama wa kikanda

3 Agosti 2022

Wanadiplomasia wakuu wa Jumuiya ya Mataifa ya Kusini Mashariki mwa Asia, ASEAN wanakutana katika mji mkuu wa Cambodia kuzidisha juhudi ya kukomesha ongezeko la vurugu nchini Myanmar.

https://p.dw.com/p/4F4rQ
Kambodscha | ASEAN Gipfeltreffen
Picha: Heng Sinith/AP/picture alliance

Mkutano huu ni wa kwanza wa ana kwa ana wa Jumuiya ya Mataifa ya Kusini Mashariki mwa Asia unaowaleta pamoja mawaziri wa mambo ya nje wa Mataifa ya Asia tangu kuzuka kwa janga la COVID-19, ambalo limedhoofisha uchumi na diplomasia. 

soma Biden akutana kwa mara ya kwanza na viongozi ASEAN

Aidha mkutano huu unajiri wakati mvutano kati ya Marekani na China unaendelea kufukuta, pamoja na kupanda kwa bei za chakula na nishati kimataifa kufuatia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Tahadhari kubwa itaelekezwa kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi na mwenzake wa Marekani Antony Blinken ambao wote wanatarajiwa kuhudhurua mkutano huu kwa mazungumzo ya usalama wa kikanda.

soma Umoja wa Ulaya umeiwekea vikwazo Myanmar

Kutuliza migogoro

Kambodscha l ASEAN-Treffen in Phnom Penh
Picha: Vincent Thian/AP/picture-alliance

Msemaji wa ASEAN Kung Phoak, ambaye pia ni naibu waziri wa mambo ya nje wa Cambodia, alisema mkutano huo utalenga kutuliza hali.

Akizungumza na waandishi wa habari Phoak amesema mawaziri watajaribu kutafuta njia ambazo jumuiya hiyo inaweza kusaidia ili hali ya Taiwan iwe shwari, na haitaleta mzozo au kuongeza joto la kisiasa kati ya pande zote zinazohusika.

''Tunatumai kuwa pande zinazohusika hazitachukua hatua zinazozorotesha au kuzidisha mivutano hiyo na sidhani kama kuongezeka kwa mivutano hiyo kutazisaidia kutatua matatizo au kutatua tofauti zilizopo. Ninasisitiza tena hitaji la pande zote zinazohusika kuzingatia kanuni hizi zote za msingi ili tuweze kuhakikisha kwamba ujia wa Bahari wa Taiwan utakuwa sehemu ya amani ya eneo hili."

Cambodia kwa sasa inashikilia uwenyekiti wa kupokezana wa jumuiya ya ASEAN, ambayo pia inajumuisha Ufilipino, Malaysia, Indonesia, Laos, Singapore, Thailand, Vietnam na Brunei pamoja na Myanmar.

Myanmar yalaaniwa kwa mauwaji

Kambodscha | Premierminister Hun Sen
Picha: Heng Sinith/AP Photo/picture alliance

Waziri Mkuu wa Cambodia, Hun Sen, akiufungua mkutano kama mwenyekiti wa ASEAN, aliilaani Myanmar kwa kuwanyonga wafungwa wanne mwezi uliopita kinyume na maombi ya kimataifa ya kutaka wahuhurumiwe.

soma Umoja wa Mataifa waikosoa Myanmar kuhusu demokrasia

Sen amesema umoja huo umekatishwa tamaa na kufadhaishwa na mauaji na kuonya kwamba matumizi zaidi ya adhabu ya kifo itamaanisha kutafakari upya mpango wa amani wenye vipengele vitano uliokubaliwa mwaka jana na Myanmar.

ASEAN, ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikidhihakiwa kama mbwa anayebweka bila meno inatoa nafasi kwa tawala za ukandamizaji, hadi sasa imeongoza juhudi zisizo na matunda za kurejesha amani.