1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAustralia

ASEAN yaonyesha hofu juu ya amani bahari ya China Kusini

6 Machi 2024

Viongozi wa ASEAN pamoja na wa Australia wameonya leo dhidi ya hatua zinazotatiza amani kwenye bahari ya China Kusini wakati msimamo unaozidi kuwa mkali wa China ukizidisha wasiwasi katika kanda hiyo.

https://p.dw.com/p/4dDMa
Australien | ASEAN Gipfel
Picha: Hamish Blair/AP Photo/picture alliance

Tamko la pamoja la viongozi hao lililotolewa wakati wa mkutano wa kilele wa siku tatu kati ya pande hizo mbili, limehimiza mataifa yote kujiepusha na vitendo vya upande mmoja vinavyohatarisha amani, usalama na utulivu katika kanda hiyo.

Akizungumzia kuhusu usalama wa bahari ya China Kusini, waziri mkuu wa Australia Anthony Albanese amesema,

"Nina wasiwasi na Australia ina wasiwasi kuhusu hatua yoyote isiyo salama na yakuvuruga amani katika bahari ya China Kusini. Ni hatari na inasababisha kitisho cha kuchukuliwa hatua zisizofaa ambazo zinaweza kuchangia kuongezeka kwa mvutano."

China inadai kumiliki karibu bahari yote ya China Kusini na kupuuza vielelezo vya kisheria na madai pinzani kutoka kwa mataifa mengi ya Kusini Mashariki mwa Asia.