1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ASANTE KOTOKO NA HEARTS OF OAK ZATOKA SULUHU (1:1) KATIKA FINALI YA KOMBE LA CAF.MKENYA ROBERT CHERUIYOT ASHINDA SAO PAOLO MARATHON

Ramadhan Ali3 Januari 2005
https://p.dw.com/p/CHZc

ASANTE KOTOKO NA HEARTS OF OAK ZATOKA SULUHU (1:1) KATIKA FINALI YA KOMBE LA SHIRIKISHO LA AFRIKA

-MANCHESTER UNITED NA ARSENAL ZAIONYA CHEALSEA BADO SI MABINGWA

NA MKENYA ROBERT CHERUIYOT ASHINDA MBIO ZA MWAKA MPYA ZA SAO PAULO BRAZIL

Ligi kadhaa zikiwa bado katika likizo ya X-masi na mwaka mpya pamoja na Bundesliga-Ligi ya Ujerumani, Ligi ya Uingereza-Premier League,haikusita na licha ya ushindi wa mwishoni mwa wiki wa viongozi wa Ligi Chelsea, mahasimu wake wakubwa-Manchester United na Arsenal London, zimeionya Chelsea kwamba kutangulia si kufika.Chelsea inaingia uwanjani kesho kupambana na Middlesbrough ikiwa bado inaoongoza orodha ya Ligi kwa pointi 5 mbele ya mabingwa watetezi Arsenal na imefungua mwanya wa hadi pointi 9 kutoka Manchester.

Chelsea hata hivyo, iliponea chupuchupu jumamosi ilipotoroka na ushindi wa bao 1:0 dhidi ya Fc liverpool.

Huko Ureno, stadi wa Brazil ,Roberto carlos ambae bado anavutana na klabu yake ya Real madrid ya Spain juu ya malipo,amekanusha taarifa za magazeti jana kwamba anapanga kuachana na Real .Amefichua kwamba amelikataa ombi la kumtaka ajiunge na Chelsea ya Uingereza.

Mabingwa wa Ulaya wa kombe la klabu bingwa FC porto wamearifu kwamba watawafungia kucheza wane kati ya kikosi chao cha wachezaji wa Brazil pamoja nao chipukizi Diego kwa sababu hawakurejea Ureno kwa wakati kutoka likizo za X-masi nyumbani Brazil.Diego pamoja na mshambulizi Derlei,mlinzi Pepe na wingi Maciel,walipigwa marufuku kushiriki katika mazowezi pamoja na wenzao wa timu hapo jana kwa kukawia kuwasili.

FINALI YA KOMBE LA SHIRIKISHO LA DIMBA LA AFRIKA:CAF:

Duru ya kwanza ya finali ya kombe la mashirikisho barani Afrika kati ya timu 2 za Ghana-Asante Kotoko na Hearts of Oak jana ilimalizika suluhu bao 1:1 .Klabu hizo 2 za ghana zimecheza finali ilioahirishwa mwezi uliopita wa desemba kutokana na uchaguzi wa rais wa ghana.Hii ilikua finali ya kwanza ya kinyan’ganyiro hiki kipya cha Kombe hili lililoanzishwa mwaka jana na CAF-shirikisho la dimba la Afrika.

Hearts of Oak ilikuwa mwenyeji wa duru ya kwanza ya jana ya finali hii mjini Accra na duru ya pili na ya mwisho itakayoamua hatima ya Kombe hili itachezwa mjini Kumasi wikimijayo,Januari 9.

Louis Agyeman aliipatia Hearts of Oak bao la kusawazisha dakika ya mwisho ya mchezo.

RIADHA:

Mkenya Robert Cheruiyot alinyakua mwishoni mwa wiki ushindi wa mbio za km 15 barabarni za mji wa Sao Paulo,Brazil kuamkia mwaka mpya.Huu ni ushindi wake wa pili mnamo muda wa miaka 3.Ulinzi mkali uliwekwa wakati wa mbio hizo za barabarani ambao haukuwahi kuonekana kabla.

Cheruiyot aliwakimbia wenzake pale walipopita Jengo la michezo ya kuigiza –Municipal Theatre,zikisalia km 2.5 kutoka mwisho wa mbio hizo.

Mkenya huyo alimaliza mbio hizo akigubikwa pande zote mbili na polisi waliopanda pikipiki kuzuwia ule mkasa uliompata Mbrazil De Lima katika michezo ya Olimpik ya Athens usdimkute Robert Cheruiyot.De Lima alikua anaongoza mbio za marathon za olimpik mjini Athens kabla shabiki hakumshambulia na kumzuwia kendelea na mbio. Baadae alimaliza 3 na kuondokea na medali ya shaba badala ya dhahabu.

Na taarifa kumhusu Vanderlei De Lima binafsi inasema amealikwa kushiriki katika mbio za marathon za Lake Biwa hapo machi.Binafsi De Lima amekwepa sao paulo marathon na kusubiri mbio hizo za Japan kama mbio zake za kwanza kabisa mwaka huu na tangu zile za Athens.

Tangu mkasa ule katika olimpik, De Lima, amekua maarufu nchini Brazil na ulimwengu kwa jnumla akialikwa kukimbia huku na huku na kuwa safu moja na mastadi wa dimba wa Brazil kama Ronaldo,Rivaldo na Ronaldinho.