Arusha:Kesi dhidi mtuhumiwa wa mauaji ya kiholela ya Rwanda imeanza mjini Arusha.
9 Januari 2007Matangazo
Kesi ya mwanasiasa wa cheo cha juu anayetuhumiwa kuwa ni mchochezi mkubwa wa mauaji ya kiholela ya mwaka 1994 huko Rwanda imeanza nchini Tanzania. Tharcisse Renzaho, gavana wa zamani wa mji mkuu wa Rwanda, Kigali, anakabiliwa na mashtaka kadhaa mbele ya mahakama ya kimataifa ya jinai, yakiwemo yale ya mauaji ya kiholela, kushiriki kufanya njama ya mauaji ya kiholela na kubaka. Mahakama hiyo ya Umoja wa Mataifa, ilio na makao yake mjinI Arusha, Tanzania, inajihusisha na madai kwamba Renzaho alihusika moja kwa moja na kuuliwa Watutsi na Wahutu walio na msimamo wa wstani wapatao laki nane.