Arusha: Watu wawili wamehukumiwa kifungo cha maisha na watatu ...
3 Desemba 2003Matangazo
miaka 35 jela kwa makosa ya kutumia vyombo vya habari kuchochea mauwaji ya halaiki nchini Rwanda.Habari hizo zimetangazwa na shirika huru la habari la Hirondelles lililonukuu duru za mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa vita mjini Arusha kaskazini mwa Tanzania.Ferdinand Nahimana,muanzilishi wa kituo cha matangazo ya radio na televisheni "Milles Collines na mchapichaji wa zamani wa gazeti Kangura Hassan Ngeze kila mmoja amehukumiwa kifungo cha maisha jela.Afisa mwengine wa kituo hicho cha matangazo cha RTLM Jean Bosco Barayagwiza amehukumiwa kifungo cha miaka 35 jela.