1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Arusha: Jenerali Romeo Dallaire wa Canada,aliyewahi ...

16 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFid
kuongoza tume ya umoja wa mataifa nchini Rwanda hadi mwaka 1994,atafika mbele ya korti kuu ya kimataifa mjini Arusha ,jumatatu ijayo,kutoa ushahidi katika kesi ya madhamana wanne wa jeshi la zamani la Rwanda.Hii ni mara ya pili kwa jenerali huyo aliyestaafu kuitwa mbele ya korti kuu ya uhalifu wa vita mjini Arusha.Duru za mahakama zinasema huenda jenerali Dallaire akasikilizwa kwa muda wa siku tisaa.Kesi dhidi ya wanajeshi hao iliakhirishwa december mwaka jana.Jenerali Dallaire aliwahi kutoa ushahidi katika mwaka 1998,katika kesi dhidi ya meya wa zamani wa Taba Jean Paul Akayezu,aliyehukumiwa kifungo cha maisha.Safari hii ataabidi kutoa ushahidi dhidi ya mkurugenzi wa zamani wa waziri wa ulinzi kanali Théoneste Bagosora,dhamana wa zamani wa opereshini za kijeshi brigadia jenerali Gratien Kabiligi,mkuu wa zamani wa jeshi mkoani Gisenyi lutenio kanali Anatole NSENJIYUNVA na meja ALOYS NHAPVAKUZE.Kesi yao ilianza mwezi september mwaka 2002.