1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Arusha: Dawa mpya kwa ugonjwa wa Malaria

9 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF5L

Mabingwa wa afya wanasema mmea ambao kiasili unatumiwa kupambana na homa huenda ukawa muhimu katika kupambana na ugonjwa wa Malaria. Faida ya maji yanayotokana na mmea huo, kwa jina la Wormwood na Sweet Annie, na njia za kuengeza kupatikana mmea huyo ni masuala yaliotwama katika mkutano wa Shirika la Afya Duniani, WHO, uliomalizika jana huko Tanzania. Mabingwa wa afya wanasema maelfu ya maisha yanaweza kunusurika kwa kutumia tiba inayotokana na mmea huo. Ugonjwa wa Malaria unachukuwa mamilioni ya maisha katika Afrika, Asia na Amerika ya Kusini kwa vile madawa ya vidonge ya kupambana na ugonjwa huo mara nyingi ni ghali mno.