Arsenal, AC Milan na Marseille zaingia vitani hii leo
23 Novemba 2010Timu hizo tatu, zinatafuta nafasi hiyo kuungana na Chelsea, Real Madrid pamoja na Bayern Munich ambazo tayari zimekwishafuzu kwa duru hiyo ijayo inayoshirikisha timu 16.
AC Milan ambayo inakamata nafasi ya pili katika kundi lake la G inahitaji kushinda mechi yake hii leo dhidi ya Auxerre, lakini huku ikiomba vinara Real Madrid iifunge Ajax Amsterdam.
Marseille wao wanahitaji ushindi wa bao zaidi ya moja kwa bila dhidi ya Spartak Moscow ili kujipatia tiketi hiyo. Arsenala wao ambao ndiyo vinara wa kundi lao H wakitofautiana mabao na Shakhtar Donetsk wanahitaji sare ya aina yoyote ile ili watakapoumana na Spartag Brag,Na Donetsk wataweza pia kufuzu iwapo watapata matokeo mazuri kuliko Brag.
Nayo AS Roma itaweza kufuzu tu iwapo itaifunga Bayern Munich mjini Roma hii leo, lakini wakati huo huo iombe mungu CFR Cluj and Basel zitoke sare.Bayern yenyewe imekwishafuzu, kwa duru ijayo na pengine inachohitaji ni kushinda ili kukamata uongozi wa kundi hilo.
Mechi za Kundi A,B,C na D zitafanyika kesho Jumatano
Mwandishi:Aboubakary Liongo