Kitendawili cha nani atakayekuwa kiongozi wa chama cha kihafadhina cha Kansela wa Ujerumani Angela Merkel kimeteguliwa kufuatia ushindi wa Armin Laschet ambaye ni Waziri Mkuu wa jimbo la North-Rheine Westphalia, lililopo magharibi mwa Ujerumani. Sura ya Ujerumani inaangazia será ya Laschet ya mambo ya nje itakavyoweza kuwa kuelekea bara lake la Ulaya na pia barani Afrika. Harrison Mwilima asimulia