1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHaiti

Ariel Henry ajiuzulu kama waziri mkuu wa Haiti

25 Aprili 2024

Waziri mkuu wa Haiti Ariel Henry amejiuzulu leo na kufungua njia ya kuundwa kwa serikali mpya katika taifa hilo la ambalo limekumbwa na vurugu za magenge.

https://p.dw.com/p/4fBzB
Waziri Mkuu wa zamani wa Haiti
Waziri Mkuu wa zamani wa HaitiPicha: Sean Kilpatrick/The Canadian Press/AP/picture alliance

Henry alitangaza kujiuzulu kwake kupitia barua iliyoandikwa jana na kutiwa saini mjini Los Angeles nchini Marekani, ambayo imetolewa leo na ofisi yake katika siku ambapo baraza lililopewa jukumu la kumchagua waziri mkuu mpya pamoja na baraza la mawaziri linatarajiwa kuapishwa.

Baraza hilo litaanza kazi zaidi ya mwezi mmoja baada ya viongozi wa eneo la Caribbean kutangaza kuundwa kwake kufuatia mkutano wa dharura wa kukabiliana na mzozo unaoendelea nchini Haiti.