You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Yanayoangaziwa
Uchaguzi wa Marekani 2024
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Sauti zetu
Vidio zetu
Matangazo
App
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
Maoni: Usalama wa majengo Afrika Mashariki
Usalama wa Muundo: Kwa nini ni muhimu katika usanifu wa majengo na ujenzi? Je, kwa nini ni muhimu kuzingatia sana usalama wa kimuundo wa majengo kabla kuanza kutumiwa kwa shughuli za kibinadamu? Jiunge na Josephat Charo katika kipindi cha Maoni mbele ya Meza ya Duara.
21.11.2024 Matangazo ya Jioni
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC imetoa waranti wa kukamatwa Waziri Mkuu wa Israel Benyamin Netanyahu na aliyekuwa Waziri wake wa Ulinzi Yoav Gallant kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu unaodaiwa kufanywa katika Ukanda wa Gaza// Rais William Ruto ametoa hotuba ya hali ya taifa kwenye bunge la nchi hiyo.
21.11.2024 Matangazo ya Mchana
Palestina imelaani hatua ya Marekani ya kuzuia azimio la kusitishwa kwa mapigano huko Gaza katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa//Baadhi ya vyama vya upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo vimeungana pamoja, ili kupinga mpango wa Rais Félix Tshisekedi, wa kubadilisha katiba ya nchi hiyo.
21.11.2024 Matangazo ya Asubuhi
Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki IAEA, Rafael Grossi amesema Iran imekubali ombi la kuzingatia kurutubisha hadi asilimia 60 ya madini ya Urani na kutovuka kiwango hicho// Matukio ya ukatili dhidi ya wanawake majumbani yaliongezeka nchini Ujerumani mwaka uliopita.
21.11.2024 Taarifa ya Habari Asubuhi
Mkuu wa shirika la kimataifa la Atomiki akaribisha uamuzi wa Iran kuhusu mpango wake wa nyuklia // Ukraine yaripotiwa kufyatua ndani ya Urusi makombora yaliyotengenezwa na Uingereza // Na Waziri Mkuu wa Mali afutwa kazi baada ya kuukosoa utawala wa kijeshi
20.11.2024 Matangazo ya Jioni
Sikiliza Dunia Yetu Leo Jioni 20.11.2024 kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW, Bonn.
20.11.2024 Matangazo ya Mchana
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Kura nyingine ya Baraza la Usalama la UN kuhusu Gaza/ Mke wa kiongozi wa upinzani Uganda asema mumewe anashikiliwa kwenye jela moja nchini Kenya.
20.11.2024: Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Rais wa Ukraine amesema Marekani ikipunguza ufadhili wake, Kiev itashindwa vita dhidi ya Moscow. +++ Mjumbe wa Marekani anayehusika na Mashariki ya Kati aeleza kuwa makubaliano ya kusitisha vita kati ya Israel na kundi la Hezbollah yanakaribia kufikiwa. +++ Upinzani nchini Msumbiji kuomboleza vifo vya watu 50 waliouawa kufuatia ghasia za baada ya uchaguzi.
19.11.2024 Matangazo ya Jioni
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amesema leo kuwa mwaka 2025 ndio mwaka utakaoamua ni nani atakayeshinda vita vinavyoendelea nchini mwake//Mwenyekiti wa chama kikuu cha Upinzania nchini Tanzania, CHADEMA, Freeman Mbowe amesema mifarakano ndani ya chama hicho ni jambo la kawaida// Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars imefuzu kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2025.
19.11.2024 Matangazo ya Mchana
Ukraine imesema kuwa itaendelea kupambana na kuzuia uvamizi wa Urusi leo ikiwa zimetimia siku elfu moja tangu Kremlin kuamrisha vikosi vyake kuingia nchini humo//Mpatanishi wa Marekani katika mzozo wa Mashariki ya Kati Amos Hochstein, amewasili mjini Beirut leo Jumanne //Mkutano wa kilele wa kundi la nchi tajiri na zilie zinazoinukia kiuchumi la G20 unaingia siku ya pili leo.
18.11.2024 Matangazo ya Jioni
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Serikali ya Tanzania yaahidi kuimarisha juhudi za uokozi wa wahanga wa ajali ya jengo/ Umoja wa Ulaya umesema utaongoza ufadhili wa kukabili mabadiliko ya tabianchi kwenye nchi maskini
19.11.2024 Matangazo ya Asubuhi
Ushindi wa Donald Trump katika uchaguzi wa rais wa Novemba 5 nchini Marekani umeambatana na chama chake cha Republican kudhibiti mabaraza yote mawili ya bunge la taifa//Wanafunzi wa vyuo vikuu kupitia viongozi wao, kwa ushirikiano na shirika la elimu linaloitwa Elimu Bora nchini Kenya, wameelezea changamoto mbali mbali zinazowakabili.
19.11.2024: Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Ukraine imesema kuwa uamuzi wa Marekani wa kuiruhusu kutumia makombora yake ya masafa marefu kushambulia ndani ya Urusi, unaweza kubadili mwelekeo wa vita. Viongozi wa G20 waliokusanyika nchini Brazil wametoa wito wa usitishwaji vita Gaza na Lebanon huku wakihimiza amani nchini Ukraine. Urusi yapinga kwa kura ya turufu azimio la Umoja wa Mataifa la kusitisha mapigano nchini Sudan.
18.11.2024 Matangazo ya Mchana
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Marekani yaruhusu Ukraine kutumia makombora yake ya masafa marefu ndani ya Urusi/ Mkutano wa G20 kufunguliwa mjini Rio, Brazil
Mkutano wa G20 kufunguliwa mjini Rio, Brazil
Mizozo inayoshuhudiwa ulimwenguni inatarajiwa pia kugubika majadiliano ya mkutano wa G20 mjini Rio de Janeiro.
18.11.2024 Matangazo ya Asubuhi
Katika matangazo yetu ya asubuhi hivi leo utasikia makala zetu za Mbiu ya Mnyonge, Makala yetu Leo, Mtu na Mazingira, Vijana Tugutuke na Jukwaa la manufaa
18.11.2024: Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Rais Joe Biden airuhusu Ukraine kutumia makombora ya masafa marefu ya Marekani kushambulia ndani ya Urusi. Chama tawala nchini Senegal chadai kupata ushindi katika uchaguzi wa Bunge. Afisa mawasilino wa Hezbollah Mohammed Afif auawa kufuatia shambulio la Israel.
Matangazo ya Jioni. 17.11.2024
Wakuu wa nchi wameanza kuwasili mjini Rio de Janeiro kuhudhuria mkutano wa G20. Utawala wa taliban wataka upewe misaada na jumuiya ya kimataifa. Waokoaji waendelea kuwasaka manusura katika jengo lililoporomoka jijini Dar es Salaam.
Waokoaji waendelea kuwatowa watu kwenye vifusi Dar es Salaam
Vikosi vya uokozi vinaendelea kuwasaka manusura wa ajali ya kuporomoka kwa jengo katika jiji kuu la kiuchumi la Tanzania
Mkutano wa G20 waanza
Wakuu wa nchi wameanza kuwasili mjini Rio de Janeiro leo Jumapili kuhudhuria mkutano wa G20.
Senegal wachaguwa wabunge wapya
Wapigakura zaidi ya milioni saba wanawachagua wabunge 165 kuhudumu kwa kipindi cha miaka mitano.
Matangazo ya Mchana 17.11.2024
Rais wa China Xi Jinping akutana na Rais wa Marekani Joe Biden. Urusi yaishambulia Ukraine kwa makombora na ndege zisizo na rubani. Kimbunga Man-yi chapiga nchini Ufilipino.
15.11.2024 Matangazo ya Jioni
Maafisa wa Umoja wa Mataifa wamesema hali bado inasuasua katika ufikishaji wa misaada kwenye Ukanda wa Gaza //Viongozi wa SADC wakijiandaa kukutana katika mji mkuu wa Zimbabwe, Harare, kuangazia mzozo wa Msumbiji.
CHADEMA yamjibu Lissu, makada wake kuhusu madai ya rushwa
Chama Kikuu cha Upinzani Tanzania, CHADEMA, kimejitokeza hadharani kujibu tuhuma kali zilizoibuliwa na makada wake.
15.11.2024 Matangazo ya Mchana
Chama Kikuu cha Upinzani Tanzania CHADEMA kimejitokeza hadharani kujibu tuhuma kali zilizoibuliwa na makada wake // Wanaharakati wa tabianchi leo wamefanya maandamano mjini Baku nchini Azerbaijan //Rais wa Marekani Joe Biden na mwenzake wa China Xi Jinping wamewasili nchini Peru kwa mkutano wa kilele wa Jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi wa nchi za Asia-Pasifiki, APEC.
Wanaharakati wa tabianchi wafanya maandamano mjini Baku
Wadau wakuu katika sekta ya mafuta leo wamehudhuria mkutano wa kilele wa mazingira wa Umoja wa Mataifa COP29 mjini Baku.
15.11.2024 Matangazo ya Asubuhi
Donald Trump anatarajiwa kuapishwa mnamo mwezi Januari kuingia tena Ikulu lakini bado anakabiliwa na kesi kwenye majimbo na pia kitaifa. Jee nini kitatokea?// Jumuiya ya wanafunzi walio na ulemavu katika taasisi za elimu ya juu imetoa kilio kwa watungaji sera katika mataifa ya mashariki mwa Afrika.
14.11.2024 Matangazo ya Jioni
Azerbaijan, mwenyeji wa mkutano wa mazingira wa Umoja wa Mataifa COP29, leo imejaribu kupunguza joto la kidiplomasia mjini Baku baada ya waziri wa mazingira wa Ufaransa Agnes Pannier-Runacher kufutilia mbali ziara yake nchini humo// Leo Novemba 14, 2024 ni siku ya Kimataifa ya kukabiliana na ugonjwa wa Kisukari.
14.11.2024 Matangazo ya Mchana
Rais mteule wa Marekani Donald Trump jana Jumatano aliwasili katika Ikulu ya White House kwa mara ya kwanza tangu aliposhinda uchaguzi wa wiki iliyopita// Mkuu wa shirika la kimataifa la nishati ya Atomiki IAEA Rafael Grossi amekutana leo na mwanadiplomasia mkuu wa Iran Abbas Araghchi// Zaidi ya watu wazima milioni 800 wanaugua ugonjwa wa kisukari duniani kote.
14.11.2024 Matangazo ya Asubuhi
Mkutano wa kila mwaka wa Umoja wa Mataifa juu ya Mabadiliko ya Tabianchi, COP29, unaendelea katika mji mkuu wa Azerbaijan, Baku// Kuporomoka kwa ushawishi wa Marekani barani Afrika kunamaanisha kuwa, utawala wa Rais mteule Donald Trump utapaswa kupambana na changamoto kadhaa katika kulielewa bara hilo
13.11.2024 Matangazo ya Jioni
Marekani kuipa Ukraine misaada zaidi kabla ya Trump kuingia madarakani/ Kongo yakabiliwa na uhaba wa chanjo ya Mpox
13.11.2024 Matangazo ya Mchana
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Jeshi la Israel leo hii Jumatano limewaaamuru wakaazi wa sehemu za vitongoji vya kusini mwa Beirut kuondoka/ Biden na Trump kukutana Whitehouse kujadili makabidiano ya madaraka
Israel yauwa wengine sita Lebanon
Mashambulizi ya Israel nchini Lebanon yameuwa watu sita na Marekani ikishambulia maghala ya Hizbullah nchini Syria.
13.11.2024 Matangazo ya Asubuhi
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Mashambulizi ya mabomu na uvamizi wa ardhini wa Israel nchini Lebanon yamesababisha zaidi ya watu milioni moja kuyahama makazi yao/ Ziwa Victoria limetajwa kama chanzo kikuu cha ugonjwa wa Kichocho nchini Kenya
13.11.2024: Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Taarifa ya Habari ya Asubuhi ya leo ina mengi lakini makubwa ni: Rais mteule wa Marekani Donald Trump aendelea kufanya teuzi, akiunda serikali yake mpya: Marekani yazizuia ndege za kiraia kwenda Haiti baada ya ndege moja kushambuliwa ilipokuwa inaingia Haiti: Na Somaliland yafanya uchaguzi wa rais katikati ya mzozo wa kidiplomasia. Sikiliza zaidi.
12.11.2024 Matangazo ya Jioni
Israel inaendeleza mashambulizi huko Gaza na nchini Lebanon// (Rais mteule wa Marekani, Donald Trump, ametangaza wajumbe wapya wa serikali yake inayokuja//Wadau wa elimu barani Afrika wamejumuika jijini Dar es Salaam leo kujadili changamoto na fursa mbalimbali za kuimarisha mifumo ya elimu.
12.11.2024 Matangazo ya Mchana
Takriban mataifa 200 yamekusanyika katika mkutano wa kila mwaka wa Umoja wa Mataifa juu ya Mabadiliko ya Tabianchi, COP29// Viongozi wa mataifa ya Kiarabu na Kiislamu waliokutana jana nchini Saudi Arabia, wametoa wito wa usitishwaji vita huko Gaza na nchini Lebanon huku wakisisitiza kwamba kuondoka kwa Israel katika maeneo ya Palestina.
Tunatafuta Neno la Mwaka 2024
Shiriki katika kura ili kusaidia kuamua Neno la Mwaka 2024 na upate bahati ya kushinda seti ya DW
12.11.2024 Matangazo ya Asubuhi
Warepublican, ambao wana mipango mikubwa, huenda wataongoza Ikulu ya White House na mabunge yote mawili ya Congress//Umoja wa Mataifa umesema ushawishi wa waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda katika sehemu za mashariki mwa Kongo sasa umeongezeka//Mkutano wa 29 wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP29) unafunguliwa rasmi hii leo mjini Baku, Azerbaijan.
11.11.2024 Matangazo ya Jioni
Mkutano wa kilele wa kila mwaka wa Umoja wa Mataifa kuhusu mazingira, unaendelea Baku nchini Azerbaijan// Jeshi la Polisi Zanzibar linasema linafanya uchunguzi wa vifo vya watu wawili vilivyotokea kaskazini mwa kisiwa cha Unguja vinavyohusishwa na vikosi vya usalama.
11.11.2024 Matangazo ya Mchana
Urusi na Ukraine zimeshambuliana usiku wa kuamkia leo// Mkutano wa kilele wa kila mwaka wa Umoja wa Mataifa kuhusu mazingira, umeanza leo mjini Baku nchini Azerbaijan// Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema yuko tayari kuitisha kura ya imani juu yake katika mwaka huu wa 2024 iwapo pande zote zitaridhia ili kuwezesha kuitishwa uchaguzi wa mapema.
11.11.2024 Matangazo ya Asubuhi
Katika matangazo yetu ya asubuhi hivi leo utasikia makala zetu za Mbiu ya Mnyonge, Makala yetu Leo, Mtu na Mazingira, Vijana Tugutuke na Jukwaa la manufaa. Sikiliza ya Dunia Yetu Leo Asubuhi kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW Bonn.
11.11.2024: Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Ungana nasi hapa kusikiliza Taarifa ya Habari ya Asubuhi, ambapo miongoni mwa mengineyo utasikia Rais mteule wa Marekani Donald Trump afanya mazungumzo na Rais Vladimir Putin wa Urusi: Haiti yamteua Waziri Mkuu mpya, hatua inayotishia mzozo zaidi kwenye taifa hilo la kisiwa: Na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz aashiria utayari wa kuitisha mapema kura ya imani ya bunge.
Matangazo ya Jioni 10.11.2024
Dunia yetu leo Jioni 10.11.2024
Droni 62 kati ya 45 za Urusi zadunguliwa Ukraine
Jeshi la anga la Ukraine mapema leo limesema limezidungua droni 62 kati ya 145 zilizorushwa na Urusi nchini humo.
Qatar yajiondowa upatanishi vita vya Gaza
Qatar imejiondowa kwenye upatanishi wa kusaka makubaliano ya kusitisha vita vya Gaza na kuachiliwa kwa mateka.
Waasi wauwa 26 Baluchistan
Mashambulizi ya bomu yaliyofanywa na kundi linalopigania kujitenga nchini Pakistan yameuwa watu 26.
Makala ya Afrika Wiki Hii
Amina Abubakar ana mengi katika Makala ya Afrika Wiki hii, ikiwemo kile kinachoendelea Marekani, Donald J Trump kurejea tena madarani kama rais wa 47 wa taifa hilo. Je ushindi wake una maana gani kwa Bara la Afrika? Nchini Msumbiji ghasia za baada ya uchaguzi zashuhudiwa na Kongo na Rwanda zathibitisha haja ya kuheshimu usitishaji mapigano mashariki mwa Kongo.
Viongozi wa Ulaya waahidi mageuzi ya kiuchumi
Viongozi wa Umoja wa Ulaya waliokutana Budapest, Hungary wameahidi kuufanyia mageuzi ya haraka uchumi wa kanda hiyo.
08.11.2024 Matangazo ya Jioni
Viongozi wa Ulaya wameungana na Israel na Uholanzi kulaani vurugu zilizoibuka baada ya mechi kati ya timu za Maccabi Tel Aviv na Ajax ya Amsterdam+++Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch (HRW) limesema watu wapatao 30 wameuawa nchini Msumbiji.
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 2 wa 130
Ukurasa unaofuatia