1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Anwaar-Ul-Haq anatarjiwa kuapishwa kuwa waziri mkuu

14 Agosti 2023

Pakistan leo inajiandaa kumuapisha ,Anwaar-Ul-Haq kuwa waziri mkuu wa mpito atakayeisimamia nchi hiyo kuandaa uchaguzi mpya unaotarajiwa kufanyika miezi kadhaa ijayo.

https://p.dw.com/p/4V8Vm
Pakistan | Anwaar ul Haq Kakar wird neuer Interims-Premierminister
Picha: Banaras Khan/AFP/Getty Images

Anwaar Kakar mwenye umri wa miaka 52 ni seneta asiyejulikana sana nchini humo na ameteuliwa kushikilia nafasi hiyo wakati Pakistan ikikabiliwa na mkwamo wa kisiasa na ukosefu wa uthabiti wa kiuchumi kwa miezi sasa,huku waziri mkuu wa zamani aliyeondolewa kwa nguvu madarakani na bunge,Imran Khan akiwa jela.Mwanasiasa huyo amezuiwa kugombea uchaguzi kwa miaka 5. Kakar ataapishwa leo ikiwa pia ni siku ya uhuru wa Pakistan na sherehe hiyo itaoneshwa moja kwa moja kwenye televisheni.Jukumu lake la kwanza litakuwa ni kuteua baraza la mawaziri.