1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Annan amkazia sauti Assad

3 Juni 2012

Mjumbe wa amani wa kimataifa Kofi Annan ameyashutumu majeshi ya rais wa Syria Bashar al-Assad kwa mauaji pamoja na kuwakamata watu kinyume na sheria .

https://p.dw.com/p/1576R
epa03240405 A handout picture released by Syrian Arab news agency (SANA), shows Syrian president Bashar al-Assad (R) meeting with the UN international envoy Kofi Annan in Damascus, Syria, 29 May 2012. According to media reports on 29 May, French President Francois Hollande announced the expulsion of Syria's ambassador to France. The move comes in response to last week's attack bombardment of the city of Houla, in which more than 100 civilians dozens of them children died. EPA/SANA HANDOUT BEST QUALITY AVAILABLE HANDOUT EDITORIAL USE ONLY/NO SALES +++(c) dpa - Bildfunk+++
Kofi Annan akizungumza na Bashar al AssadPicha: picture-alliance/dpa

Annan , ambaye  ameteuliwa  kuwa  mjumbe  maalum  nchini  Syria na  umoja  wa  mataifa  pamoja  na  umoja  wa  mataifa  ya  Kiarabu, Arab League, amesema  uwezekano  wa  kutokea  vita  vya wenyewe  kwa  wenyewe  unakuwa  mkubwa   kila  siku  na  kutia wasi  wasi  mataifa  mengine  ya  mashariki  ya  kati.

Hali  hiyo  ya  hofu ,  inaongezeka  kutokana  na   kuuwawa  kwa watu  tisa  na  wengine  42  wamejeruhiwa  katika  mapigano  kati ya  watu  wanaomuunga  mkono  Assad  na  wale  wanaompinga ambao  wameshambuliana  kwa  silaha  kali  na  makombora  katika nchi  jirani  ya  Lebanon , katika  mji  wa   bandari  wa Tripoli.

Katika  mkutano na  viongozi  wa  umoja  wa  mataifa  ya  Kiarabu , Annan  ametoa  tathmini  yenye  kuonyesha  hali  isiyoridhisha nchini  Syria  miezi  15  tangu  kuanza  kwa  vuguvugu  la maandamano  dhidi  ya  Assad  na  wiki  moja  baada  ya  mauaji  ya zaidi  ya  watu  100  ambayo  waangalizi  wa  amani  wa  umoja  wa mataifa  wanayalaumu  majeshi  ya   rais Assad.

In this image made from amateur video released by the Shaam News Network and accessed Monday, May 28, 2012, purports to show black smoke rising from buildings in Homs, Syria. U.N. envoy Kofi Annan called Monday on "every individual with a gun" in Syria to lay down arms, saying he was horrified by a weekend massacre that killed more than 100 people, including women and small children. (Foto:Shaam News Network via AP video/AP/dapd) TV OUT, THE ASSOCIATED PRESS CANNOT INDEPENDENTLY VERIFY THE CONTENT, DATE, LOCATION OR AUTHENTICITY OF THIS MATERIAL
Majengo yakishambuliwa nchini SyriaPicha: dapd

Assad  ni  lazima  achukua   hatua  madhubuti  zinazoonekana haraka  kubadilisha  msimamo  wa  majeshi  yake  na  kutekeleza majukumu  yake  na  kuondoa  majeshi  yake katika  maeneo  ya raia  na  kuacha  matumizi  yote  ya  nguvu  dhidi  ya  raia, amesema Annan , ambaye  amekutana  na  kiongozi  wa  Syria  mjini Damascus siku  ya  Jumanne.

Kitu  muhimu  sio  maneno  anayotumia  lakini  hatua  anazochukua hivi  sasa, amesema  mjumbe  huyo  maalum, na  kuongeza  kuwa ujumbe  wake  kwa  Assad umekuwa , ni  wa  moja  kwa  moja  na wa  wazi.

A team of U.N. monitors walk through a hotel in Damascus April 16, 2012. A United Nations advance observers' team arrived in the Syrian capital Damascus late Sunday to monitor the fragile cease-fire brokered by international envoy Kofi Annan, causing discussion from all circles in Syria. REUTERS/Khaled al- Hariri (SYRIA - Tags: CIVIL UNREST MILITARY POLITICS)
Waangalizi wa amani wa umoja wa mataifa nchini SyriaPicha: Reuters

Annan , ambaye  amekuwa  akizuru  eneo  hilo, amesema  kuwa uwezekano  wa  kutokea  vita  vya  wenyewe  kwa  wenyewe, na kuleta  hofu  ya  kuzuka  kwa mapambano  ya  kimadhehebu, inaongezeka  kila  siku.

Hisia  zangu  zinaambatana  na  wasi  wasi  wa  nchi  jirani  ya  Syria na  nimezionyesha  katika  majadiliano  yangu  ya  hivi  karibuni.

Waziri  mkuu  wa  Lebanon  Najib  Mikati  amekwenda   haraka  mjini Tripoli  kiasi  ya  kilometa  70  kaskazini  mwa  Beirut , kujaribu kuzuwia  ghasia  katika  eneo  hilo. Jeshi  limeingia  katika  eneo  hilo likiwa  na   magari  ya  deraya  lakini  hayakufyatua  risasi.

Vifo  vilivyotokea  siku  ya  Jumamosi  ni  idadi  ya  juu  kabisa katika  siku  moja  mjini  Tripoli, na  kuzusha  hofu  kuwa  ghasia nchini  Syria  zinaweza  kusambaa  hadi  katika  nchi  hiyo  jirani.

Mwandishi : Sekione  Kitojo /rtre

Mhariri: Sudi Mnette