Annan aita uchunguzi katika mradi wa mafuta kwa chakula.
20 Machi 2004Matangazo
NEW YORK:
Kufuatana na shutuma za ulaji rushwa katika
ule mradi kuhusu ‚mafuta badala ya chakula'
nchini Iraq, Katibu Mkuu wa UM Kofi Annan
ametangaza utafanyika uchunguzi kamili. Vyombo
vya habari vimeripoti kuwa mtawala wa zamani wa
Iraq Saddam Hussein akishirikiana na makampuni
ya Kimagharibi wameiba pesa biliyoni kadha za
UM katika biashara za rushwa. Mradi huo wa
"mafuta badala ya chakula' uliomalizika
Novemba, uliiruhusu Iraq iuze kiwango fulani
cha mafuta yake kuiwezesha kuununulia umma wake
chakula na madawa.