1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANKARA:Majeshi ya Uturuki yanaendeleza juhudi ya kuwasaka waasi wa PKK

30 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7BK

Majeshi ya Uturuki bado yanaendelea na operesheni ya kuwasaka waasi wa Kikurdi karibu na milima ya maeneo ya mpakani na Irak.

Helikopta za jeshi la Uturuki zimeshambulia maeneo yanayoaminiwa kuwa ni ya waasi wa Kikurdi katika jimbo la Sirnak kusini mashariki mwa Uturuki.

Wanajeshi wanne wa Uturuki wameuwawa katika mapigano ya siku mbili zilizopita dhidi ya waasi hao wa PKK.

Kiongozi wa KIkurdi Massud Barzani amesema kuwa hatapokea amri kutoka Uturuki inayomtaka kuwasaka na kuwamaliza waasi wa Kikurdi wanaojificha katika jimbo lake.