1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ankara. Jeshi lashambulia Wakurdi ndani ya Iraq.

7 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBu4

Uturuki imekanusha ripoti kuwa majeshi yake yamefanya shambulio kubwa ndani ya eneo la kaskazini la Iraq, na kuwalenga wapiganaji wa Kikurdi.

Mashirika ya habari yakimkariri afisa mmoja wa jeshi la Uturuki ambaye hakutajwa jina yanasema kuwa kumekuwa na operesheni ya kijeshi ndani ya mpaka wa Iraq.

Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni nchini Marekani ameitaka Uturuki kuchukua tahadhari.

Kiasi cha waasi 4,000 wa chama kilichopigwa marufuku cha Kurdinstan Workers Party , PKK, wanasemekana kuwa wamejificha nchini Iraq.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Uturuki Abdullah Gul ameieleza ripoti hiyo ya uvamizi wa wanajeshi wapatao 50,000 kuwa ni upotoshaji wa habari.

Wakati huo huo rais mpya wa Ufaransa Nikolas Sarkozy anapanga kuzuwia juhudi za Uturuki kujiunga na umoja wa Ulaya , akisema kuwa nchi hiyo kubwa haihusiani na eneo la Ulaya.