1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Angola kuuzika upya mwili wa Savimbi

21 Mei 2019

Mabaki ya mwili wa aliyekuwa kiongozi wa waasi wa Angola, Jonas Savimbi, yatazikwa tena kwenye mji wake wa Lopitanga mwezi ujao.

https://p.dw.com/p/3Ip1J
Jonas Savimbi Rebellenführer Angola SW
Picha: AP

Taarifa iliyotolewa jana (Mei 20) na Waziri wa Nchi Pedro Sebastiao ilieleza kuwa mazishi hayo yangelifanyika baada ya vipimo vya vinasaba kuthibitisha kuwa mabaki hayo ni ya Savimbi.

Savimbi, ambaye alipigana dhidi ya serikali ya kisoshalisti ya Angola katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 27, aliuawa tarehe 22 Februari 2002 katika mapambano dhidi ya vikosi vya MPLA.

Kifo chake kilifungua njia ya kufikiwa makubaliano ya amani ambayo yaliumaliza mmoja kati ya mizozo ya muda mrefu kabisa barani Afrika, ambao ulizuka baada ya Angola kupata uhuru wake kutoka Ureno mwaka 1975.

Savimbi alizikwa siku moja baada ya kuuawa katika jimbo la mashariki la Moxico.

Vipimo vya vinasaba vilivyofanyika katika maabara za Afrika Kusini, Argentina, Ureno na Angola vilithibitisha kuwa mabaki hayo ni ya mwili wa Savimbi.