1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Angela Merkel atetea Mshikamano wa Ulaya

16 Desemba 2015

Kansela Angela Merkel amelihutubia bunge mjini Berlin akishadidia mshikamano wa Umoja wa Ulaya na juhudi za kupambana na ugaidi. Hotuba ya Kansela imetolewa siku moja kabla ya mkutano wa kilele wa Umoja wa ulaya.

https://p.dw.com/p/1HOKe
Kansela Merkel akihutubia bungeni Berlin kabla ya mkutano wa kilele wa Umoja wa UlayaPicha: picture-alliance/dpa/R. Jensen

Kansela Angela Merkel amekumbusha changamoto zilizoukabili Umoja wa Ulaya mnamo mwaka huu wa 2015 na kutilia mkazo jukumu la Umoja wa Ulaya katika kuhifadhi mafanikio ya umoja huo na hasa uhuru wa watu kwenda wakutakako na sarafu ya pamoja.

Kansela Merkel anasema tnanukuu:"Tumelazimika kushuhudia changamoto zilizoutikisa mara kadhaa mshikamano barani Ulaya mwaka huu. Nna amini kwamba hasa Ujerumani,nchi muhimu zaidi kiuchumi barani Ulaya,inabidi ijibebeshe jukumu maalum wakati huu. Na ni jukumu letu kuhifadhi na kulinda mafanikio yaliopatikana katika kuzileta pamoja nchi za Umoja wa Ulaya. Kwangu mie mafanikio muhimu ni pamoja na uhuru wa watu kwenda wakutakako na sarafu ya pamoja. Kuhifadhiwa mafanikio hayo ni kwa masilahi ya dhati ya mataifa yetu."

Ujerumani inapigania mshikamano ndani ya Umoja wa ulaya

Kansela Angela Merkel amegusia pia juhudi za kupambana na na ugaidi na suala la wakimbizi. Amewaonya washirika ndani ya Umoja wa Ulaya dhidi ya hatari ya kurejea katika janga la kupigania utaifa. Amesema "kujifungia katika karne ya 21 sio njia inayofaa."Kansela Merkel anasema ugaidi,mabadiliko ya tabia nchi,na jinsi ya kukabiliana na mzozo wa wakimbizi ni masuala yatakayoweza kufumbuliwa kwa ushirikiano tu."Ndio maana katika wakati huu mgumu watu wasijaribu kujitafutia ufumbuzi wa kitaifa tu" amesema kansela Merkel.

Deutschland Bundestag Debatte und Abstimmung zum Syrien-Einsatz der Bundeswehr
Mjadala wa bunge kabla ya kuidhinishwa mpango wa ktuumwa wanajeshi wa Ujerumani kusaaidia kupambana na wanamgambo wa dola la kiislam nchini SYriaPicha: Getty Images/S. Gallup

Itafaa kusema hapa kwamba mkutano wa siku mbili wa kilele wa Umoja wa Ulaya unaoanza kesho mjini Brussels utazungumzia suala la wakimbizi na madai ya Uingereza ya kuganyiwa mageuzi ya kina Umoja wa Ulaya.

Ujerumani itachangia katika juhudi za kupambana na magaidi wa IS

Katika suala la kupambana na ugaidi kansela Merkel ametoa wito wa ushirikiano akitaja umuhimu wa kuimarishwa utaratibu wa kubadilishana ripoti za upelelezi kati ya nchi wanachama.Kansela Merkel amesema Ujerumani iko tayari kutokana na maombi ya Ufaransa,kusaidia katika kupambana na wanamgambo wa dola la kiislamu nchini Syria. Utayarifu huo umefungamana na juhudi za kupatikna ufumbuzi wa kisiasa-"Kipa umbele ni kukomesha vita nchini Syria,tena bila ya Assad" amesema kansela Merkel katika hotuba yake bungeni.

Deutschland Tornado Syrien-Einsatz der Bundeswehr
Ndege ya kivita ya Ujerumani chapa TornadoPicha: Reuters/F. Bimmer

Mwandishi:Hamidou Oumilkheir/dpa/

Mhariri . Mohammed Abdul-Rahman