Amri ya kutotoka nje Biafra
13 Septemba 2017Matangazo
Amri hiyo ya kutotoka nje, ambayo itatekelezwa kuanzia saa kumi na mbili jioni hadi saa kumi na mbili asubuhi, ilitangazwa na gavana wa jimbo la Abia, ambaye aliwaambia wakazi kubakia majumbani mwao ili kuepusha aina yoyote ya makabiliano na vikosi vya usalama au jeshi.
Kumeshuhudiwa vurugu katika siku za karibuni kati ya wafuasi wa kundi la watu wa asili ya Biafra - IPOB, ambalo linadai uhuru wa kundi la kabila kubwa la Igbo, na jeshi.
Jumapili iliyopita kundi la watu wa Biafra lilidai kuwa wanachama wake watano waliuawa madai yaliyopuuziliwa mbali na jeshi kuwa ya "uwongo mtupu".