1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Amri ya kutoandamana kubatilishwa Ethiopia

14 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEub

Addis Ababa:

Amri ya watu kutokusanyika iliyowekwa na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Meles Zenawi, haitarefushwa tena itakapomalizika juma hili. Amri hiyo ilitangazwa baada ya watu kuandamana mjini Addis Ababa mara baada ya uchaguzi mkuu uliofanywa mwezi wa Mei na kurefushwa mwezi uliopita baada ya mauaji kutokea mjini humo. Waziri wa Habari wa Ethiopia, Berekat Simon amesema kuwa kwa vile mambo yameanza kutulia na uhasama nao umeanza kupungua hakuna haja ya kurefusha tena muda wa amri hiyo. Meles Zenawi amepiga marufuku maandamano yote ya Umma mjini Addis Ababa na vitongoji vyake kwa muda wa mwezi mmoja mara baada ya vituo vya uchaguzi kufungwa Mei 15 na kurefushwa tena Juni 13 baada ya machafuko kutokea mjini humo. Waandamanaji wameipuuza amri hiyo na kulalamika kuwa uchaguzi haukuwa huru na wa haki. Watu wasiopungua 40 wameuawa wakati wa mapambano hayo kati ya Polisi na Waandamanaji.