Mali ichunguze vifo vya raia kufuatia mashambulizi ya droni
6 Novemba 2024Matangazo
Mauaji yalitokea katika mashambulizi ya droni kaskazini mwa nchi hiyo ambako jeshi linapambana na waasi wenye itikadi kali na makundi ya wanaotaka kujitenga.
Amnesty imesema mashahidi waliripoti kwamba takribani raia wanane, wakiwemo watoto sita, waliuawa katika mashambulizi ya anga kwenye soko lenye shughuli nyingi katika kijiji cha Inadiatafane, eneo la Timbuktu, mnamo Oktoba 21.
Soma pia:Sudan hali ni mbaya na hakuna ishara ya vita kumalizika
Taarifa hiyo imeongeza kuwa watu wengine 15 walijeruhiwa. Shirika hilo la kutetea haki za binaadamu pia limesema shambulizi hilo linapaswa kuchunguzwa kama uhalifu wa kivita kwa sababu lilisababisha vifo na majeruhi miongoni mwa raia huku miundombinu ya kiraia pia ikilengwa