Amina malkia wa Zazzau aliibuka katika wakati ambapo maisha yalikuwa yakitawaliwa na wanaume. Alikuwa ni shujaa wa kabila la Hausa. Aliongoza jeshi kubwa la wanaume ambalo lilivamia na kudhibiti maeneo mengi, hali iliyomuwezesha kuupanua ufalme wake. Alifungua njia za biashara na kuulinda mji wake kwa kuuzungushia kuta.