1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Amama Mbabazi kugombea urais Uganda

Emmanuel Lubega31 Julai 2015

Aliyekuwa waziri mkuu wa Uganda na pia katibu mkuu wa chama tawala nchini humo cha NRM, Amama Mbabazi, ametangaza kwamba atagombea urais katika uchaguzi wa mwaka ujao kama mgombea binafsi.

https://p.dw.com/p/1G7ux
Amama Mbabazi, waziri mkuu wa zamani wa Uganda
Picha: picture-alliance/AP Photo/A. Zemlianichenko

Hatua hiyo ameichukua siku ya mwisho kwa wenye nia ya kugombea urais kwa ktiketi ya NRM kuchukua fomu, yaani ijumaa hii. Ijumaa ilikuwa siku ya mwisho kwa wanachama wa NRM kuwasilisha maombi ya uteuzi na rais Museveni mwenyewe anatarajiwa kufanya hivyo. Alikuwa miongoni mwa wale waliolipa ada mwanzoni mwa zoezi hilo lakini Mbabazi alisusia kufanya hivyo akipinga malipo hayo pamoja na kwamba alitaka kuoneshwa kanuni na masharti ya kugombea tiketi ya urais.

Mbabazi kuchukuliwa hatua za kinidhamu?

Kwa upande wake rais Museveni amewasilisha rasmi maombi yake na kueleza kuwa Uganda ingali inamhitaji kutekeleza mipango kabambe ya maendeleo.
Museveni amesema hayo kwenye makao makuu ya chama hicho ambapo ameshangiliwa na halaiki ya wafuasi wake. Hata hivyo huenda Mbabazi atachukuliwa hatua za kinidhamu mwa maamuzi take lakini Ana haki mwa mujibu wa katiba ya nchi kugombea wadhifa wa urais bila kudhaminiwa na chama chochote.

Kizza Besigye agombea kwa mara ya nne
Kizza Besigye agombea kwa mara ya nnePicha: Getty Images/AFP/I. Kasamani

Hadi kufikia sasa, viongozi kadhaa wametangaza kutaka kugombea urais. Dr Kizza Besigye kwa mara ya nne anataka kugombea kwa tiketi ya FDC lakini itambidi kupata hakikisho hilo iwapo atamshinda rais wa chama hicho kwa sasa meja jenerali Mugisha Muntu katika uchaguzi wa ndani ya chama. Norbert Mao wa DP pamoja Profesa Venansius Baryamureba ni wanasiasa wengine ambao wameanza kujinadi kukabiliana na rais Museveni ambaye ametawala Uganda kwa takribani miaka thelathini.