New Zealand washinda Kombe la Dunia la Rugby
2 Novemba 2015New Zealand iliishinda Australia kwa pointi 34-17 katika fainali ya Jumamosi uwanjani Twickenham.
Carter mwenye umri wa miaka 33, ambaye pia alishinda tuzo huyo mwaka wa 2005 na 2012, alipata pointi 19 katika fainali ya Jumamosi na akatajwa mchezaji bora wa mchuano huo katika kile kilikuwa ni mchuano wake wa 112 na wa mwisho wa kimataifa.
Carter anajiunga na nahodha wa All Blacks anajiunga na nahodha Ritchie McCaw kama washindi mara tatu wa tuzo hiyo maridadi kabisa ambayo washindi wake wengine wa awali ni pamoja na Thierry Dusautoir, Bryan Habana wa Afrika Kusini na Jonny Wilkinson.
New Zealand pia imepewa tuzo ya Timu Bora ya Mwaka baada ya kuwa nchi ya kwanza kufanikiwa kuhifadhi Kombe la Dunia. Kocha wa Australia Michael Cheika alipokea tuzo ya Kocha Bora wa Mwaka baada ya kuyanoa makali ya timu ya Wallabies katika uongozi wake wa miezi 12, na kuwaongoza hadi fainali ya Kombe la Dunia.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters
Mhariri: Yusuf Saumu