1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Algiers:Kura ya maoni juu ya mpango wa amani Algeria.

29 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEWZ

Waalgeria wanapiga kura ya maoni leo, yenye lengo la kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha zaidi ya watu 100,000 kuuwawa. Ikiwa waraka wa amani na upatanishi wa kitaifa unaopigiwa kura utapitishwa, utatoa msamaha kwa wengi miongoni mwa waliohusika na vifo hivyo. Lakini utawatenga wale waliokua dhamana wa mauaji, ubakaji na mashambulio ya kigaidi.

Wapinzani wanasema, waraka huo unafunika maovu ya miaka mingi ya mauaji na ukandamizaji wa haki za binaadamu, pamoja na kumpa Rais madaraka mpya makubwa zaidi. Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilianza 1992, baada ya jeshi la Algeria kuufuta uchaguzi, ambapo wanaharakati wa kiislamu wa msimamo mkali wakielekea kushinda.