ALGIERS: Wananchi wa Algeria wakumbuka mauaji ya 1945
9 Mei 2005Matangazo
Waalgeria wameandamana katika mji wa Setif mashariki mwa nchi,kukumbuka mauaji ya maelfu ya wapinzani waliopigania uhuru,miaka 60 ya nyuma.Wanahistoria wa Algeria wanasema askari jeshi wa Ufaransa waliwaua watu 45,000 walipotumia nguvu kuyavunja maandamano ya Setif tarehe 8 Mei mwaka 1945.Nchini Ufaransa,wageni wenye asili ya Kialgeria na Kimoroko wapatao mia kadhaa waliandamana mjini Paris,kuadhimisha siku hiyo ya ukumbusho.Waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa,Michel Barnier hapo kabla alitoa muito kwa serikali za Paris na Algiers zisaidiane kukabiliana na enzi hiyo ya maumivu katika historia yao ya pamoja.