ALGIERS : Waalgeria wachaguwa bunge jipya
17 Mei 2007Matangazo
Wananchi wa Algeria wanapiga kura leo hii kulichaguwa bunge jipya.
Huu ni uchaguzi wa tatu wa bunge tokea kufutwa kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 1992 ambao ulichochea uasi wa Kiislam ambapo chama cha siasa kali za Kiislam ambacho sasa kimepigwa marufuku kilitazamiwa kushinda uchaguzi huo.
Usalama umeimarishwa kwa ajili ya uchaguzi huu ambao unafanyika siku moja baada ya kuuwawa kwa afisa mmoja wa polisi na wengine watano kujeruhiwa baada ya bomu kuripuka katika mji wa Constantine na kuzusha hofu ya kurudia kwa umwagaji damu wa kisiasa ulioshuhudiwa katika miaka ya 1990 ambapo zaidi ya watu 200,000 waliuwawa.