ALGIERS: Ujerumani itapata gesi ziada kutoka Algeria
17 Novemba 2006Matangazo
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier alipokuwa ziarani nchini Algeria alisema Algeria itaipatia Ujerumani gesi iliyofanywa maji maji.Amesema gesi hiyo itakuwa ziada ya ile gesi inayonunuliwa kutoka Urussi. Duru za biashara za Ujerumani zimesema,rais Abdelaziz Bouteflika wa Algeria vile vile anataka msaada wa ujuzi wa uhandisi wa Ujerumani kupanua miundo mbinu pamoja na biashara na kupunguza kutegemea nishati.Waziri Steinmeier,baada ya kukamilisha ziara yake nchini Algeria,alielekea Tunesia ambako alitoa mwito wa kufanywa mageuzi ya kidemokrasia.