ALGIERS : Maandamano dhidi ya mashambulizi ya mabomu
10 Septemba 2007Matangazo
Takriban Waalgeria 5,000 wamekuwa na maandamano ya amani katikati ya Algeria kufuatia mashambulizi mawili ya kujitolea muhanga kwa kujiripuwa siku chache zilizopita ambayo yameuwa watu wapatao 50.
Maandamano mengine madogo pia yalifanyika katika miji mengine ya Algeria.Tawi la Al Qaeda katik nchi hiyo ya Afrika Kaskazini limelaumiwa kwa mashambulizi hayo.Takriban watu 30 wameuwawa hapo Jumamosi kwenye kambi ya walinzi wa mwambao katika bandari ya Dellys mashariki mwa Algiers wakati lori lilosheheni mabomu liliporipuka.Hapo Alhamisi watu 20 wameuwawa wakati mshambuliaji wa kujitolewa muhanga maisha alipojiripuwa kwenya umati wa watu uliokuwa ukimsubiri Rais Abdelaziz Bouteflika aliyekuwa akizuru eneo hilo.