ALGIERS: Kundi la waasi lajihusisha na mashambulio ya mabomu
12 Aprili 2007Matangazo
Kundi la waasi lenye mafungamano na kundi la kigaidi la Al Qaeda limetangaza kwamba lilihusika na mashambulio mawili ya mabomu ya kujitoa muhanga katika mji mkuu wa Algiers nchini Algeria.
Watu 24 waliuwawa na wengine zaidi ya 222 walijeruhiwa katika milipuko hiyo.
Kundi hilo la kiisalmu la Maghreb limetoa tangazo la kuhusika kwake kwa njia ya simu kupitia televisheni ya kiarabu ya Al Jazeera.
Mlipuko wa kwanza ulitokea mbele ya ofisi ya waziri mkuu wa Algeria, Abdulaziz Belkhadem.
Shambulio la pili lilienga kituo cha polisi katika eneo la mashariki mwa mji mkuu wa Algiers.