1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Algiers. Israel yakataa maazimio ya mkutano wa jumuiya ya Kiarabu ya kurejeshewa maeneo yaliyotekwa na Israel katika vita.

23 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFUH

Viongozi wa mataifa ya Kiarabu jana waliidhinisha azimio la kufufua juhudi za kuleta amani kuielekea Israel katika msingi kwamba ardhi zote za Waarabu zinazokaliwa na Waisrael zirejeshwe pamoja na kuundwa kwa taifa la Palestina, lakini azimio hilo lilikataliwa mara moja na Israel.Waziri wa mambo ya kigeni wa Jordan Hani Mulki amesema kuwa mkutano huo wa viongozi wa Kiarabu umepitisha maazimio yote, mojawapo likiwa lile la kufufua juhudi za kuleta amani za Mataifa ya Kiarabu.

Alikuwa akizungumza wakati viongozi hao wa Kiarabu wanamaliza siku moja ya mkutano wao wa siku mbili katika mji mkuu wa Algeria ambao umekumbwa na hatua ya baadhi ya viongozi muhimu kutohudhuria, ikiwa ni pamoja na mfalme wa Jordan Abdullah wa pili ambaye alikuwa akitafuta kuungwa mkono zaidi juhudi hizo za kuleta amani.

Kiongizi wa Saudi Arabia mwanamfalme Abdullah bin Abdul Aziz alijitoa katika mkutano huo katika dakika za mwisho, ndie aliyewasilisha mpango huo katika mkutano uliofanyika Beirut mwaka 2002 na ukaidhinishwa, lakini ulikataliwa mara moja pia na Israel.