1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ALGIERS: 13 wafa katika mlipuko wa gesi

20 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFhf

Kwa uchache watu 13 wameuawa katika mlipuko wa kituo kimoja cha mafuta ya petroli na gesi nchini Algeria na kusababisha uharibifu mkubwa wa vifaa. Taarifa za serikali zinasema kuwa ajali imetokea katika kiwanda cha Skikda ambacho ndio kikubwa kabisa cha mafuta na gesi nchini Algeria. Watu wengine wapatao 74 wanatajwa kuwa wamejeruhiwa pia katikma mlipuko huo, ambao kwa mujibu wa waziri wa nishati Chakib KHELIL, unaendelea kutoa moto mkubwa ingawa hatua zimechukuliwa kuzuwia kutapakaa maeneo jirani na sehemu hiyo.