Algeria yapitisha sheria ya kupandisha kodi
23 Novemba 2016Matangazo
Wengi wa wabunge wa chama tawala Algeria waliuidhinisha mswada huo hapo jana huku wabunge wa upinzani wakisusia kura hiyo.
Mohamed Djemai, mbunge wa chama tawala cha National Liberation Front, amesema ameunga mkono mswada huo kwani hauathiri mafao ya kimsingi ya kijamii ya Waalgeria, licha ya matatizo ya kiuchumi.
Wanaoupinga mswada huo, wakiwemo walimu na wahudumu wa afya nchini humo, wamepanga kufanya maandamano kuanzia tarehe 27 hadi 29 mwezi huu.
Mabadiliko katika bajeti yatapelekea kuanzishwa kwa kodi mpya na kuongezwa kwa bei za tumbaku, pombe na mafuta.
Wakosoaji wa mswada huo wanaishutumu serikali na matajiri kwa kujilimbikizia mali nyingi, ilhali wananchi wa kawaida wakitaabika na mfumko wa bei.