Algeria yafunga anga lake kwa ndeze za Morocco
23 Septemba 2021Ofisi ya rais wa Algeria, imesema uamuzi huo umekuja kufuatia uchokozi unaoendelea na vitendo vya uhasama kwa upande wa Morocco.
Ufungaji huo wa anga unahusisha pia ndege zote zenye nambari za usajili za Morocco, ilisema ofisi ya rais baada ya mkutano wa baraza la usalama.
Hakukuwa na tamko rasmi kutoka Morocco juu ya kadhia hiyo.
Lakini chanzo kutoka shirika la Royal Air Maroc, kilisema ufungaji huo utaathiri safari 15 tu za ndege kila wiki, zinazoiunganisha Morocco na mataifa ya Tunisia, Uturuki na Misri.
Algeria ilivunja uhusiano na Morocco mwezi uliyopita, ikitaja kile ilichokiita matendo ya kiuadui kutoka Morocco, ikimaanisha hasa matamshi yaliotolewa na balozi wa Morocco mjini New York, yaliounga mkono uhuru wa eneo la Kabylie nchini Algeria.