ALEY Muungano wa upinzani waashindwa katika awamu ya tatu ya uchaguzi wa bunge nchini Lebanon
13 Juni 2005Matangazo
Muungano wa upinzani nchini Lebanon, ulioongoza kampeni ya kuwalazimisha wanajeshi wa Syria kuondoka nchini humo, umeshindwa kwenye kila eneo la kikristo, katika awamu ya tatu ya uchaguzi wa bunge uliyofanyika nchini humo.
Kiongozi wa wakristo anayeipinga Syria, Michel Aoun, ambaye sasa ameunda muungano na vyama vya washiriki wa Syria, alijinyakulia viti vingi katika maeneo ya mlima Lebanon na eneo la mashariki la bonde la Bekaa, dhidi ya wapinzani wake. Karibu nusu ya viti vyote 128 bungeni vilipiganiwa katika uchaguzi huo, hivyo kuifanya awamu hiyo ya tatu kuwa muhimu zaidi.
Kura hiyo ni ya kwanza kufanyika nchini humo tangu Syria ilipowaondoa wanajeshi wake kutoka Lebanon, baada ya kuikalia nchi hiyo kwa miaka karibu 30.