1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoUingereza

Alcaraz ambwaga nguli Djokovic na kubeba taji la Wimbledon

17 Julai 2023

Carlos Alcaraz anaamini kuwa ushindi uliotimiza ndoto yake wa taji la Wimbledon dhidi ya Novak Djokovic unaweza kuashiria mabadiliko ya utawala katika mchezo wa tenisi ya waunaume

https://p.dw.com/p/4U0HH
Wimbledon I  Carlos Alcaraz  v Novak Djokovic
Picha: Kirsty Wigglesworth/AP/picture alliance

Alcaraz alihitimisha ushindi wa Djokovic wa mataji manne mfululizo ya Wimbledon katika fainali ya kukata na shoka jana Jumapili yenye seti tano. Alishinda kwa seti za 1-6, 7-6 (8/6), 6-1, 3-6, 6-4. Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 20 alimhanganisha Djokovic kwa Zaidi ya saa nne na dakika 42 na kutwaa taji lake la kwanza la Wimbledon na taji lake la pili kuu katika taaluma yake.

Baada ya miongo miwili ya Djokovic, Roger Federer na Rafael Nadal kutawala mchezo huo, Alcaraz anasema ushindi wake huenda ukawa mwanzo wa enzi mpya. "Kusema kweli, sikuamini. Nilidhani kwamba hii ilikuwa mshtuko. Nilikuwa katika mshtuko kwa kweli. Baada ya kushinda pointi ya mwisho, ilikuwa ndoto yangu. Kuweza kufanikisha hili, kutimiza ndoto yangu katika umri wa miaka 20 kwangu, inashangaza."

Wakati Djokovic alishinda taji lake la kwanza kuu katika mashindano ya Australian Open mwaka wa 2008, Alcaraz alikuwa anakaribia umri wa miaka mitano. Alcaraz, ambaye alishinda taji lake la kwanza la Grand Slam katika mashindano ya US Open mwaka jana, amempiku Mserbia Djokovic katika orodha ya karibuni ya wachezaji bora ulimwenguni.

afp