Al-Shabab yenye mafungamano na Al-Qaeda imetoa taarifa jana ikitishia kufanya shambulio "ndani ya moyo wa Kenya" iwapo serikali ijayo haitaondoa wanajeshi wa Kenya nchini Somalia. Al-Shabab imesema imeionya serikali ya Kenya kuwa hatua ya wanajeshi wake kuivamia Somalia itakuwa na madhara makubwa. Sudi Mnette amezungumza na mjuzi wa masuala ya usalama wa Kenya, Enoc Makanga kuhusu kitisho hicho.