1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Al-shabab wavuruga amani nchini Somalia

Admin.WagnerD21 Juni 2013

Watu tisa,wakiwemo raia watatu na wafanyakazi wa tatu wa Umoja wa Mataifa wameuawa katika mashambulizi ya al-shabab yaliolenga jengo la Umoja wa Mataifa mjini Mogadishu, huku Duru za hospitali zikisema watu 18 wamekufa

https://p.dw.com/p/18tRT
Jengo la UN mjini Mogadishu
Jengo la UN mjini MogadishuPicha: Reuters

Baraza la usalama la Umoja wa mataifa limelaani mashambulizi hayo ambayo ni makubwa kuwahi kushudiwa katika miaka ya hivi karibuni dhidi ya taasisi za kimataifa ndani ya Somalia.

katika mashambulizi yaliodumu kwa muda saa moja na nusu katika jengo la Umoja wa mataiafa, kwa uchache raia wa kigeni pamoja na wakandarasi wawili raia wa Afrika kusini wameuawa pamoja na wasomlia kadhaa wanaofanya kazi Umoja wa Mataifa nchini humo.

Wapiganaji saba wa al-sahabab waliuawa wakati umoja wa Afrika na vikosi vya serikali ya Somlia vikichukua udhibiti wa jengo hilo katika mashambulizi ya zaidi ya saa moja.

Waziri wa mambo ya ndani wa Somalia Abdulkareem Husein amesema vikosi vya Somalia vikisaidiwa na vile ya umoja wa Afrika,vinaimarisha ulinzi katika jengo hilo la umoja wa mataifa.

Msemaji wa Umoja wa mataifa nchini Somalia Nicholas Kay amesema hali ya wafanyakazi wa umoja wa mataifa ni salama na tayari wamehamishwa wote kwenda eneo la uwanja wa ndege wa Mogadishu ambalo ina ulinzi mkubwa wa vikosi vya umoja wa Afrika.

Kwa upande wao wapiganaji wa kundi la al-shabab wamedai kuhusika na shambulio hilo ambalo walitumia gari lililobeba mabomu na watu wa kujitoa muhanga kwa lengo la kuvamia jengo la umoja wa mataifa karibu na uwanja wa ndege wa Mogadishu.

Msemaji wa baraza la usalama la taifa kutoka mjini Washington Marekani Caitlin Hayden amesema shambulio hilo linakumbusha vitendo vya kigaidi vinavyochukiza vinavyoendelezwa na wapiganaji wa al-shabab ili kukwamisha juhudi za kumaliza machungu ya raia wa Somalia.

Kwa upande wake Baraza la usalama la umoja wa mataiafa limesema vitendo hivyo vya kigaidi vya al-shabab haviwezi kuzuia azma yake ya kuisaidia Somalia katika kipindi hiki cha mpito cha kuelekea katika amani na uthabiti

Katika maazimio hayo yaliotolewa kwa pamoja na wajumbe 15 wa baraza la usalama la umoja wa Mtaifa, wameahidi kundeleza juhudi za kupambana na watu wanaotaka kuvuruga amani na utengamano nchini Somalia.

Mbali na hilo wajumbe hao wa baraza la usalama la umoja wa mataifa wameahidi kuwasaidia wafanyakazi wa umoja wa mataifa ambao wanafanya kazi Sonalia kwa ajili ya kulinda amani,uthabiti na maendeleo kwa raia wa Somalia.

Mashambulizi hayo yanarudi wakati Somalia ilikuwa ikitumia kipindi hiki cha utulivu kuwavutia watoa misaada wa kimataifa na mashirika mengine ya kimataifa kurudi nchini Somalia.

Mwandishi: Hasimu Gulana/DPAA & DPAE

Mhariri: Abdul-Rahman Mohammed