Al-Shabaab yawashambulia AMISOM
25 Oktoba 2016Mshambuliaji huo aliripua lori lake kwenye lango la kambi katika mji wa Beledweyne, wanakoishi wanajeshi kutoka Djibouti.
Msemaji wa kijeshi wa al-Shabab, Sheikh Abdulaziz Abu Musab, amesema wanajeshi wea Djibouti wamelengwa, kama kisasi vitendo vinavyokiuka madili, na mauaji vilivyofanywa na wanajeshi hao.
Umoja wa Afrika baadaye ulituma ujumbe kupitia mtandao wa Twitter, ukisema washambuliaji wapatao 10 wameuawa wote.
Rais Hassan Sheikh Mahamoud wa Somalia ameyalaani mashambuliuzi hayo, akisema wale aliowaita maadui wa amani walikuwa wakiazimia kusababisha mtafaruku ndani ya nchi yake.
Licha ya kunyang'anywa ngome zake nyingi, kundi la al-Shabab ambalo lina mafungamano na mtandao wa kigaidi wa al-Qaida, limekuwa likiendelea kuvishambulia vituo vya Umoja wa Afrika na vya serikali ya Somalia.