Al-Shabaab yauwa tena Mandera
25 Oktoba 2016Kundi la kigaidi la al-Shabaab kutoka Somalia limedai kuhusika na mashambulizi hayo, likidai kupitia kituo chake cha redio cha Andalus, kwamba waliouawa ni 15.
Chanzo cha polisi kimeliambia shirika la habari la AFP kuwa waliopoteza maisha ni wanaume 11 na mwanamke mmoja, waliokuwa katika nyumba ya wageni ya Bisharo katika Kaunti ya Mandera.
Hii ni mara ya pili kwa al-Shabaab kufanya mashambulizi katika Kaunti ya Mandera katika muda wa wiki tatu. Mashambulizi mengine ya tarehe 6 mwezi huu wa Oktoba yaliuawa watu sita katika jengo ambalo linakaliwa zaidi na watu wasiokuwa na asili ya Kisomali na wasiokuwa Waislamu.
Taarifa za hivi punde zimeeleza kuwa al-Shabab imefanya mashambulizi mengine katika kambi ya walinzi wa amani wa Umoja wa Afrika katika eneo la Baledweyne nchini Somalia.