Al-Shabaab waukimbia mji wa Mogadishu
6 Agosti 2011Rais Sharif Sheikh Ahmed wa Somalia ameahidi kwamba majeshi yake yatarejesha amani na utengemano katika mji wa Mogadishu baada ya wapiganaji wa al-Shabaab kurejea nyuma na kuondoka kutoka mji mkuu huo alfajiri ya leo, baada ya kujiri masaa kadhaa ya mapigano. Aliuwambia mkutano wa waandishi wa habari katika kasri yake inayolindwa vikali kwamba ni wakati sasa wa kuvuna matunda ya amani. Rais huyo, ambaye mwenyewe alikuwa mwanachama wa kikundi cha Kiislamu ambacho kilidhibiti sehemu za nchi hiyo hapo zamani, alitoa mwito kwa raia kuwaariffu wakuu wa serekali juu ya harakati zozote za wapiganaji wa Kiislamu wanaojificha katika mji huo.
Waziri mkuu wa Somalia, Abdiweli Mohamed Ali, alihakikisha kwamba mji huo ulikuwa unadhibitiwa kwa mara ya kwanza baada ya kupita miaka na serekali yake ilio dhaifu, na kwamba wataendelea kuwafyeka al-Shabaab katika mikoa yote.