Kulingana na Shirika la Afya Duniani – WHO, matukio ya ugonjwa wa Preeclampsia yani kifafa cha mimba huwa kati ya asilimia 2 hadi 10 kipindi cha ujauzito kote duniani huku asilimia 1.8 hadi 16.7 yakiripotiwa katika mataifa yanayokua kiuchumi na mataifa yaliyoendelea yakirekodi asilimia 0.4 ya matukio haya.