Afrika yapambana na mabadiliko ya tabianchi
Hakuna bara lililoathirika na mabadiliko ya tabianchi kama Afrika. Lakini nchi zilizoathirika hazitaki kungoja. Zimezindua zenyewe mipango ya kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi
Afrika yapambana na mabadiliko ya tabianchi
Mengi ni mataifa ya kiviwanda ambayo huchangia katika mabadiliko ya tabianchi kwa kutoa gesi ya mkaa. Waathiriwa aghalabu ni nchi za kusini. Waafrika hawataki kusimama tu na kutazama kiangazi, vimbunga, mmomonyoko na ueneaji wa majanga vikiharibu mataifa yao. Katika miaka ya karibuni, yameanzisha mipango ya kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi
Wakimbizi milioni 20 wa mabadiliko ya tabianchi kutoka Afrika?
Mjini Beira, Msumbiji, watu tayari wanahisi athari za mabadiliko ya tabianchi. Kupanda kwa kiwango cha bahari – mafuriko yanaharibu vitongoji vyote. Kwa mujibu wa Greenpeace, watu wengi hukimbia mara mbili Zaidi kila mwaka kuliko vita na mahafuko. Wataalamu wanatabiri kuwa huenda kukawa na wakimbizi milioni 20 wa mabadiliko ya tabianchi kutoka Afrika katika miaka kumi ijayo
Kuzikabili nguvu za bahari
Shirika la IPCC linakadiria kuwa viwango vya bahari vitapanda kwa sentimeta 40 hadi 80 ifikapo 2020. Lakini mji wa Beira hautaki kuzama kwenye mafuriko. Mifereji mipya na vizuizi vya ku mawimbi vimejengwa kuyalinda maeneo ya hatari mjini humo. Kukiwa na mawimbi makubwa, milango ya vizuizi hufunguliwa ili kuulinda mji. Wakati wa mvua kubwa, maji yanaweza kupita vizuri
Ukuta wa kijani barani Afrika
Jangwa la Sahara linaendelea kuenea barani Afrika, na kuharibu ardhi ya kilimo. Nchi 1 za Kiafrika zinataka kusitisha ueneaji wa jangwa kwa kuweka ukanda wa msitu wa umbali wa kilomita 7750 na upana wa kilometa 15. Watu wapate maisha mapya. Watalaamu wanauona mradi huo kuwa hatua muhimu ya kimataifa kwa ajili ya kulinda hali ya hewa
Kuzuia mmomonyoko wa udongo
Wakulima wengi hawawezi tena kufanya kilimo kwenye mashamba yao kwa sababu ya mmomonyoko na ueneaji wa jangwa. Kwa kutumia mfumo maalum wa unyunyiziaji, Sounna Moussa kutoka Niger anaufanya udongo wake uwe na rutuba tena. Mbinu yake ni ya karne nyingi zilizopita, lakini imesahaulika kabisa. Watalaamu wanapendekeza kupanda mimea Zaidi ya kiasili badala ya kilimo cha aina moja ya mmea
Umeme wa maji badala ya makaa ya mawe
Hata mataifa makubwa ya kikoloni yalijenga mabwawa Afrika. Serikali nyingi za Kiafrika pia huwekeza katika umeme wa maji ili kuhakikisha kuna nishati ya kutosha katika nchi zao. Mabwawa mapya bado yanajengwa. Umeme wa maji hauathiri hali ya hewa. Hata hivyo, miradi mingine ni tata: Aghalabu misitu yote ya kuvutia mvua hukatwa au jamii za vijijini kuhamishwa
Nishati safi barani Afrika
Ifikapo 2030, kona ya mwisho kabisa ya Afrika itakuwa na umeme. Lengo hili kubwa liliwekwa na viongozi 55 wa mataifa na serikali za kiafrika katika Kongamano la Mabadiliko ya Tabianchi la Paris mwaka wa 2015. Mpango wa nishati mbadala barani Afrika unalenga kutoa gigawati 300 za nishati safi kwa mwaka katika gridi ya umeme wa Afrika. Mitambo ya nishati ya upepo kama hapa Ethiopia ni mwanzo tu
Kujitegemea
Watu wengi sana Afrika wanajitafutia umeme na hawategemei tena usambazaji wa umeme kutoka kwa serikali. Paneli za umeme wa jua vya bei nafuu husaidia nishati safi kupatikana kwa unafuu. Watu wengi binafsi hawategemei tena jenereta, bali hutumia nishati ya jua. Mashirika ya misaada yanafanya maendeleo katika shule na hospitali zinazotumia nishati ya jua, au taa.
Chupa za plastiki badala ya matofali
Barani Afrika, mtindo wa kutumia upya vitu vilivyotumika haujauteka tu ulimwengu wa mitindo. Nchini Nigeria mtu hujenga nyumba nzima kwa kutumia chupa za zamani. Hakuna mfumo wa kutupa vitu vilivyotumika au kutupa taka huko. Karne nyingi zingepita kabla ya chupa hizo kuoza. Chupa hizo hujazwa udongo au mawe na kushikanishwa na udongo. Hivyo zinachukua nafasi ya matofali ambayo ni bei ghali
Shujaa chipukizi wa hali ya hewa Tanzania
Getrude Clement aliye na umri wa miaka 16 kutoka Tanzania amejitolea kuyalinda mazingira. Mara moja kwa wiki hutengeneza kipindi cha mazingira katika kituo cha redio cha mji anaotokea. “Natumai wasikilizaji wangu wanafanya kitu ili kubadilisha hali hapa – kuyalinda mazingira na kuyaweka maji safi”. Aprili 2016, alizungumza katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York
Wataalamu wa hali ya hewa wanahitaji Afrika
Ili kuchukua hatua dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi, rekodi za data lazima ziundwe. “Kituo cha Sayansi cha Mabadiliko ya Tabianchi na Matumizi Mbadala ya Ardhi Kusini mwa Afrika” kinashughulikia hili. Angola, Botswana, Namibia, Afrika Kusini, Zambia na Ujerumani zilianzisha kituo hicho. Kinalenga kuzuia athari za mabadiliko ya tabianchi kwa kilimo na maji katika kanda hiyo