Miongoni mwa matukio tuliyoyatupia jicho katika Afrika wiki hii ni pamoja na mchakato wa kuandikisha wagombea katika uchaguzi wa serikali za mitaa, ambako wapinzani walia kuchezewa rafu na chama tawala huku wakitangaza kujiondowa kwenye uchaguzi huo. Nchini Burundi nako wapinzani pia walia kwa kuonewa na kuandamwa kuelekea uchaguzi mkuu lakini pia hali sio shwari ndani ya chama tawala CNDD-FDD.