Taasisi ya Kimataifa inayojihusisha na utendaji kazi wa vyombo vya habari duniani, Freedom House, inayaweka mataifa ya Afrika Mashariki katika kigawe kinachoanzia kwenye yale yasiyo kabisa na uhuru wa habari hadi yale yenye aina fulani ya uhuru wa habari. Je, hii ina maana gani katika uhalisia wa waandishi wa habari, wale hasa ambao wanaishi na kuziishi habari zenyewe?