1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi ya kigaidi Afrika Magharibi yapindukia 1800

26 Julai 2023

Rais wa Kamisheni ya Jumuiya ya Uchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, Omar Touray, amesema Afrika Magharibi imerekodi zaidi ya mashambulizi 1,800 ya kigaidi katika miezi sita ya kwanza ya mwaka 2023.

https://p.dw.com/p/4UOaa
BG I Alltag und Militarismus in Cabo Delgado
Picha: Roberto Paquete/DW

Rais wa Kamisheni ya Jumuiya ya Uchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, Omar Touray, amesema Afrika Magharibi imerekodi zaidi ya mashambulizi 1,800 ya kigaidi katika miezi sita ya kwanza ya mwaka 2023. Touray ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba mashambulizi hayo yamesababisha takribani vifo 4,600 na mzozo wa kiutu.

Ukosefu wa usalama kwenye eneo la ECOWAS unasababishwa na ugaidi

Amesema hiyo ni sehemu ndogo tu ya madhara ya kutisha ya ukosefu wa usalama. Kwa mujibu wa Touray, watu nusu milioni katika mataifa 15 ya ECOWAS ni wakimbizi na takribani milioni 6.2 ni wakimbizi wa ndani, huku watu milioni 30 wakihitaji msaada wa chakula. Amesema ukosefu wa usalama kwenye eneo la ECOWAS unasababishwa na ugaidi, uasi wa kutumia silaha, uhalifu uliopangwa, mabadiliko ya serikali kinyume na katiba, shughuli haramu za baharini, mizozo ya mazingira na taarifa za uongo.