Afrika Kusini yaishtaki Israel ICJ kwa 'mauaji ya kimbari'
30 Desemba 2023Kwa mujibu wa taarifa, kesi hiyo katika ICJ inahusiana na madai ya ukiukaji wa Israel wa jukumu lake chini ya Mkataba wa Mauaji ya Kimbari, na kusema kuwa "Israel imejihusisha, inajihusisha na inatishia kushiriki zaidi katika vitendo vya mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Palestina huko Gaza".
Soma pia:Wizara ya afya Gaza yasema vifo kutokana na vita na israel vimefikia 21,320
Katika kesi hiyo, Afrika Kusini pia inasema Israel imekuwa ikichukuwa hatua '' kwa lengo la kuwaangamiza Wapalestina katika Ukanda wa Gaza kama sehemu ya kundi pana la taifa, rangi na kabila la Palestina''.
Soma pia:Mkuu wa jeshi la Israel anasema vita dhidi ya Hamas vitaendelea kwa miezi mingi ijayo
Israel imepinga mashtaka hayo, huku msemaji wa wizara yake ya mambo ya nje Lior Haiat akiandika kwenye ukurasa wa X, ambao awali ulijulikana kama twitter kwamba "Israel inakataa na kuchukizwa na kashfa inayoenezwa na Afrika Kusini na ombi lake'' kwa mahakama ya ICJ.